Theme images by MichaelJay. Powered by Blogger.

Visitors

Search This Blog



Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Youtube



Flickr Images

Like us on Facebook

Instagram

Facebook

Friday, June 8, 2018

SEMINA YA MDUDU HATARI WA MIMEA SHAMBANI KIJIJI CHA CHEMBA MKOANI DODOMA



MTAALAMU WA TAASISI YA TPRI  BW.MANENO CHIDEGE AKITOA MAFUNZO KWA WANAKIJIJI WA CHEMBA  MKOANI DODOMA KUHUSU UDHIBITI WA MDUDU MWARIBIFU WA MMEA SHAMBANI AJULIKANAYE KAMA KIWAVI JESHI.

MTAALAMU WA TAASISI YA TPRI BW MANENO CHILEGE AKIWAELEKEZA WANAKIJIJI WA CHEMBA MKOANI DODOMA JINSI YA KUTUMIA MTEGO WA KUWAUA WADUDU WAHARIBIFU WA MIMEA SHAMBANI.



Shirika la viuwatilifu Tanzania TPRI wamefanya semina ya kudhibiti wadudu  waharibifu   wa mimea shambani katika kijiji cha chemba mkoani Dodoma.

Shirika hili limehakikisha wakulipa wanapata mafunzo juu yauharibifu wa mazao zaidi ya 80 ikiwemo mahindi mpunga mtama unaotokanana mdudu hatari ajulikanaye kama kiwavi jeshi

MUHINDI ULIOHARIBIWA NA MDUDU HATARI WA MIMEA AJULIKANAYE KAMA KIWAVI JESHI


Hata hivyo wamewawezesha mabwana shamba wa kijiji hicho cha chemba kufahamu jinsi ya kumdhibiti mdudu huyo kabla ya kuathiri mimea shambani

Kwa upande wake mtaalamu wa taasisi hiyo ya TPRI bw maneno chidege ameeleza juu ya utumiaji wa viuwatilifu na kuwaasa maafisa hao kuisambaza elimu walioipata kwa wakulima katika maeneo mbalimbali.

Bw chidege ametoa ushauri na kusema kuwa wakulima hao wanapaswa kutumia viuwatilifu vilivyo sajiliwa na vinavyo uwa wadudu hatari ,kudhibiti wadudu kabla hawajaingia katika mwili wa mmea ,kutumia viuwatilifu kwa muda sahihi,kuepuka mchanganyiko zaidi ya kimoja kwenye pampu ya dawa na kutembelea shamba mara kwa mara. 


Tuesday, June 5, 2018

MAAJABU YA JENGO LA JAKAYA KIKWETE NGORONGORO TOWER

Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro imeanza kurejesha fedha za mkopo dollar million kumi na tano(15)kutoka CRDB Bank ambazo zimechukua nafasi Ya asilimia sitini na tano(65%) ya ujenzi wa jengo la Jakaya Kikwete Ngorongoro Tower.

Mkurugenzi wa NCAA Bw. Fred Manongi amesema kuwa jengo hilo ambalo linatarajiwa kukabidhiwa June 30 mwaka huu, tayari makampuni ishirini na nne(24)yakiwemo ya utalii na mashirika ya ndege yameshaomba nafasi za kupangisha katika jengo hilo na baadhi yao wameshaweka fedha Bank za miezi kadhaa ili kujihakikishia uhitaji wao.

Dr. Camilius Lekule Consultancy Office Afri-Arch Associates ambaye ndio msanifu wa jengo hilo amesema jengo hilo linalotarajiwa kudumu zaidi ya miaka mia moja(100) limejengwa kwa Manyata Concept ambao ni mfumo wa ujenzi wa nyumba za kabila la kimasai ambazo huwa ni mzunguko na lina akisi mwonekano wa hifadhi ya Ngorongoro yenye duara linaloingiza mwanga kwa juu.

Dr. Camilius amesema kuwa jengo hilo lenye glass asilimia arobaini(40%) mpaka hivi Sasa limegharimu bilioni thelathini na tano nukta saba(35.7)kati ya bilioni arobaini na tano(45)zilizopo kwenye bajeti na kudai kuwa ni mara chache sana ujenzi kufanyika kwa kiwango kilichofika bila kwenda kuomba fedha ziongezwe.

Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Meja Jen Gaudence Milanzi amesema kumekuwa na wimbi la Briefcase Tourism Operators ambapo watalii wanakosa majibu ya maswali yao hivyo kuwepo kwa one stop tourism center kutatua tatizo hilo.

Gaudence amesema kuwa ubunifu aliouona hasa wa kuwepo kwa picha mjongeo zitakazoonyesha yanayofanyika hifadhini moja kwa moja jambo hilo limempa nguvu ya kusukuma yale wanayoyataka kufanikisha lengo hilo.

Sunday, June 3, 2018

FURAHIA UTALII WA BIASHARA NA HUDUMA WANAZOTOA AICC

Ikiwa ni siku ya tatu tangu kuzinduliwa rasmi maonyesho ya Kilimanjaro fair siku ya ijumaa, huduma nyingi zinazohusiana na utalii zinaendelea kutolewa katika viwanja vya chuo cha ushirika mkoani Kilimanjaro.

Miongoni mwa wanaotoa huduma hizo ni pamoja na AICC, wanatoa ofa ya nafasi ya kupangisha ofisi, makampuni pamoja na taasisi.

Pia kwa wastani kwa kila mita ya mraba ambayo inahusisha maji, umeme, usalama wa uhakika na usafi wa maeneo AICC wanatoa huduma hizi kwa uhakika wa hali ya juu.

Lengo kubwa la AICC kutoa huduma hizi kwa wateja wao ni ili kukuza na kutoa huduma bora za utalii wa biashara kwa wateja wa kitaifa na kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kitaifa, kijamii na kiuchumi.

AICC wana matarajio makubwa moja Ikiwa kuwa mfano na kuwezesha utalii wa biashara kukuza pato la Taifa.

Ndani ya viwanja vya chuo cha ushirika banda lao lipo namba N:16 unaweza kufika na kupata huduma stahiki.

              Kwa maelezo zaidi wasiliana nao
                          +255272050181 AU
                          +255272050201
              EMAIL md@aicc.co.tz
          WEBSITE  www.aicc.co.tz.

Saturday, June 2, 2018

MAONYESHO YA TATU YA KILIMANJARO FAIR

Maonyesho ya tatu ya kilimanjaro fair yamefanyika katika viwanja vya chuo cha ushirika ambapo lengo la maonyesho hayo ni kukuza utalii wa ndani.

Maonyesho haya yamefunguliwa rasmi siku ya ijumaa tarehe 1/6/2018 na mh. Charles Mwijage na kilele chake kutarajiwa kumalizika siku ya jumamosi tarehe 9/6/2018.

Mkurugenzi msaidizi wa Kilimanjaro search and rescue Bw. Willium Mbogo ameeleza huduma zinazotolewa na SAR ikiwemo kliniki kwa wageni wanaopata matatizo pale wanapokuwa wanapanda mlima. 

Bw. Willium ameendelea kusema kuwa pamoja na huduma ya kliniki kwa wageni wanaopata matatizo wawapo mlimani lakin pia wanapima afya za wageni wao kabla ya kupanda mlima Kilimanjaro ili kuhakikisha usalama wa afya za wageni wao. 

Picha ya kwanza ni REGINAJ AIR ARUSHA katika picha ya pamoja kwenye banda lao la maonyesho ya tatu(3) ya Kilimanjaro fair  wenye matawi yao Kenya, Uganda na Tanzania ambapo shirika hili la ndege limelenga kutoa huduma ya usafiri bora na wa haraka kwa watalii mbalimbali barani Africa banda namba M:20

Picha ya pili kushoto ni Willium Mbogo ambaye ni mkurugenzi msaidizi Kilimanjaro search and rescue akitoa maelezo juu ya huduma zinazotolewa na SAR banda namba J:20

Interested for our works and services?
Get more of our update !