NA EUNICE ROBERT
Wanawake kote nchini wameaswa kujifunza matumizi sahihi ya mitandao ili kukua kiteknolojia kwani kuna umuhimu wa kutumia teknolojia kwenye karne hii ya ishirini na moja.
Akizungumza na Lens Media Tv mkurugenzi wa Zaina Foundation Bi.Zainab amesema kuwa wasichana na wanawake wamekuwa nyuma sana kwenye matumizi ya teknolojia na pia hawapewi nafasi ya kuweza kujifunza ili kujua mambo mbalimbali yanayohusu teknolojia.
Ameongeza kwa kusema kuwa endapo watapata uelewa wa jinsi ya kutumia teknolojia wanaweza kutumia kwa kusoma na kwenye maswala ya afya.
Ameendelea kusema kuwa wanatarajia kila kitu kitumike kwa kuzingatia teknolojia inavyokuwa hivyo wamefanya semina na wanawake ili kuwapa elimu hiyo ya kutumia teknolojia.
Kwa upande wake Bw.Frank Nduguru ambaye ni mmoja wa washiriki amesema kuwa wamejifunza mambo mengi kuhusu Cyber Crimes na kutumia teknolojia kwa matumizi sahihi na sio kutuma picha zisizo na maadili kwa jamii ya kitanzania.
Nae Bi,Magdalena Mhina amesema kuwa wanatarajia kuwa wasichana watajilinda kuhusiana na maswala ya uzazi ili kuweza kufikia malengo yao kwa kutumia teknolojia kwa usahihi
No comments:
Write comments