BUKOMBE.Janja ya panzi kuficha kichwa wakati mkia uko nje/madereva lipen...
NA EUNICE ROBERT
Pamoja na kikosi cha usalama barabarani kuendelea kutoza faini kwa madereva wanaokiuka sheria za barabarani lakini bado baadhi ya madereva wameendelea kukimbia kulipa faini zao na kupelekea kuwapa ugumu wa kazi kikosi hicho mkoani Arusha.
Akizungumza na Lens Media Tv mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Arusha Bw.Joseph C Bukombe amesema kuwa kwa sasa wana mashine ambayo wanaandika faini na kumpatia dereva ambapo anatakiwa kulipa ndani ya siku saba lakini pia inapunguza usumbufu kwa wananchi wanaotaka risiti kwani mashine hiyo inatoa risiti hapo hapo na kusaidia kuepuka usumbufu wa kwenda kituoni.
Ameendelea kusema kuwa kutokulipa faini kwa wakati kunapelekea dereva kulipa kiasi kikubwa kwa kupitisha muda aliopewa na kusababisha usumbufu usio wa lazima
Bw.Bukombe amehitimisha kwa kuwataka madereva kutumia vizuri elimu yao walioipata darasani ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kwa kukiuka sheria za barabarani,madereva wawe makini na pia walipe faini zao kwa wakati unaotakiwa ili kuepuka kujilimbikizia madeni ndani ya kituo cha polisi.