Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro imeanza kurejesha fedha za mkopo dollar million kumi na tano(15)kutoka CRDB Bank ambazo zimechukua nafasi Ya asilimia sitini na tano(65%) ya ujenzi wa jengo la Jakaya Kikwete Ngorongoro Tower.
Mkurugenzi wa NCAA Bw. Fred Manongi amesema kuwa jengo hilo ambalo linatarajiwa kukabidhiwa June 30 mwaka huu, tayari makampuni ishirini na nne(24)yakiwemo ya utalii na mashirika ya ndege yameshaomba nafasi za kupangisha katika jengo hilo na baadhi yao wameshaweka fedha Bank za miezi kadhaa ili kujihakikishia uhitaji wao.
Dr. Camilius Lekule Consultancy Office Afri-Arch Associates ambaye ndio msanifu wa jengo hilo amesema jengo hilo linalotarajiwa kudumu zaidi ya miaka mia moja(100) limejengwa kwa Manyata Concept ambao ni mfumo wa ujenzi wa nyumba za kabila la kimasai ambazo huwa ni mzunguko na lina akisi mwonekano wa hifadhi ya Ngorongoro yenye duara linaloingiza mwanga kwa juu.
Dr. Camilius amesema kuwa jengo hilo lenye glass asilimia arobaini(40%) mpaka hivi Sasa limegharimu bilioni thelathini na tano nukta saba(35.7)kati ya bilioni arobaini na tano(45)zilizopo kwenye bajeti na kudai kuwa ni mara chache sana ujenzi kufanyika kwa kiwango kilichofika bila kwenda kuomba fedha ziongezwe.
Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Meja Jen Gaudence Milanzi amesema kumekuwa na wimbi la Briefcase Tourism Operators ambapo watalii wanakosa majibu ya maswali yao hivyo kuwepo kwa one stop tourism center kutatua tatizo hilo.
Gaudence amesema kuwa ubunifu aliouona hasa wa kuwepo kwa picha mjongeo zitakazoonyesha yanayofanyika hifadhini moja kwa moja jambo hilo limempa nguvu ya kusukuma yale wanayoyataka kufanikisha lengo hilo.
No comments:
Write comments