Maonyesho ya tatu ya kilimanjaro fair yamefanyika katika viwanja vya chuo cha ushirika ambapo lengo la maonyesho hayo ni kukuza utalii wa ndani.
Maonyesho haya yamefunguliwa rasmi siku ya ijumaa tarehe 1/6/2018 na mh. Charles Mwijage na kilele chake kutarajiwa kumalizika siku ya jumamosi tarehe 9/6/2018.
Mkurugenzi msaidizi wa Kilimanjaro search and rescue Bw. Willium Mbogo ameeleza huduma zinazotolewa na SAR ikiwemo kliniki kwa wageni wanaopata matatizo pale wanapokuwa wanapanda mlima.
Bw. Willium ameendelea kusema kuwa pamoja na huduma ya kliniki kwa wageni wanaopata matatizo wawapo mlimani lakin pia wanapima afya za wageni wao kabla ya kupanda mlima Kilimanjaro ili kuhakikisha usalama wa afya za wageni wao.
Picha ya kwanza ni REGINAJ AIR ARUSHA katika picha ya pamoja kwenye banda lao la maonyesho ya tatu(3) ya Kilimanjaro fair wenye matawi yao Kenya, Uganda na Tanzania ambapo shirika hili la ndege limelenga kutoa huduma ya usafiri bora na wa haraka kwa watalii mbalimbali barani Africa banda namba M:20
Picha ya pili kushoto ni Willium Mbogo ambaye ni mkurugenzi msaidizi Kilimanjaro search and rescue akitoa maelezo juu ya huduma zinazotolewa na SAR banda namba J:20
No comments:
Write comments