Ikiwa ni siku ya tatu tangu kuzinduliwa rasmi maonyesho ya Kilimanjaro fair siku ya ijumaa, huduma nyingi zinazohusiana na utalii zinaendelea kutolewa katika viwanja vya chuo cha ushirika mkoani Kilimanjaro.
Miongoni mwa wanaotoa huduma hizo ni pamoja na AICC, wanatoa ofa ya nafasi ya kupangisha ofisi, makampuni pamoja na taasisi.
Pia kwa wastani kwa kila mita ya mraba ambayo inahusisha maji, umeme, usalama wa uhakika na usafi wa maeneo AICC wanatoa huduma hizi kwa uhakika wa hali ya juu.
Lengo kubwa la AICC kutoa huduma hizi kwa wateja wao ni ili kukuza na kutoa huduma bora za utalii wa biashara kwa wateja wa kitaifa na kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kitaifa, kijamii na kiuchumi.
AICC wana matarajio makubwa moja Ikiwa kuwa mfano na kuwezesha utalii wa biashara kukuza pato la Taifa.
Ndani ya viwanja vya chuo cha ushirika banda lao lipo namba N:16 unaweza kufika na kupata huduma stahiki.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nao
+255272050181 AU
+255272050201
EMAIL md@aicc.co.tz
WEBSITE www.aicc.co.tz.
No comments:
Write comments