NA EUNICE ROBERT. ARUSHA
Mwanasheria wa chama cha mapinduzi (CCM) Bw.Ngemela amesimamia zoezi la kufanya usafi katika kiwanja kilichokuwa kimetaifishwa ambacho ni mali ya chama hicho.
Akizungumza na Lens Media Television mwenyekiti wa kata ya Themi Bw.Thomas Munisi amesema kuwa hawako tayari kuendelea kuona baadhi ya viongozi kutumia mali za chama kwa njia isiyo sahihi.
Hata hivyo ameongeza kwa kusema kuwa kundi la vijana wamejitokeza kufanya usafi katika kiwanja kilichothibitishwa na mwanasheria wao Bw.Ngemela kuwa ni mali halali ya chama hicho
Aidha Bw.Thomas ameendelea kusema kuwa wamejipanga vizuri na wameeka mikakati ya kuhakikisha chama chao kinasimama imara na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.
Amehitimisha kwa kuwataka wanachama na viongozi wa chama cha mapinduzi kuwa waaminifu kwa kuzilinda mali za chama hicho.
NA EUNICE ROBERT
katibu wa TUGHE na mratibu wa TUCTA mkoa wa Arusha Bw.Samwel Magero amesema kuwa mwaka huu wanategemea kuwa na sherehe za mei mosi na wamejipanga vizuri na uongozi wa serikali na pia wameshaanza maandalizi mbalimbali kwa ajili ya sherehe hizo zinazotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Arusha.
Bw.Magero amesema kuwa wamejiandaa vyema kukamilisha sherehe hiyo na mgeni rasmi anayetarajiwa kuwepo ni raisi wa nchi Mh.John Pombe Magufuli,hivyo ametangaza rasmi kwa wananchi wa Arusha kuwa tarehe moja mwezi wa tano sherehe za mei mosi zitafanyika kitaifa mkoa wa Arusha hivyo amewataka wananchi wote waweze kushiriki katika sherehe hizo.
ameendelea kusema kuwa kabla ya mei mosi kutakuwa na maonyesho ya OSHA kuanzia tarehe ishirini na tano ambapo wataonyesha mambo mbalimbali yanayohusu mambo ya kazi na mfuko wa hifadhi ya jamii.
Bw.Magero ametoa rai kwa wananchi na wafanyakazi waweze kufika kwenye maonyesho hayo ili waweze kujifunza mambo mbalimbali watakayokuwa wameandaa
Mkuu wa wilya ya monduli ambaye pia ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa bodi mpya ya maji Ngaramtoni (NGAUWSA) Mh.Iddi Kimanta amezindua rasmi bodi mpya ya maji katika mji mdogo wa Ngaramtoni mapema hii leo.
Akizungumza katika uzinduzi huo amesema kuwa bodi,viongozi na watumishi wengine wanapaswa kuelewa na kuona huduma zikoje kwani bima zinatoka kwenye vifaa vya maji.
Kwa upande wake Bw.Lembrice ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha amesema kuwa bodi ya maji NGAUWSA itakuwa na mamlaka ya kusimamia maji katika eneo la mamlaka ya mji mdogo Ngaramtoni kwa lengo la kutoa huduma bora ya maji safi na salama.
Bw.Lembrice ameendelea kusema kuwa wanategemea kuanzishwa kwa bodi hiyo kutasaidia maeneo ambayo hakuna maji waweze kupata kwa urahisi kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo halmashauri,wananchi,serikali kuu na wadau wengine wa maendeleo kuhusiana na swala zima la upatikanaji wa maji safi na salama.
Hivyo amehitimisha kwa kusema kuwa kuzinduliwa kwa bodi hii ni kwa mujibu wa sheria hivyo watekeleze wajibu waokwa kushirikiana na wadau wengine.
Aidha meneja wa mamlaka ya maji katika mji mdogo wa Ngaramtoni Bw,Claiison Kimaro amesema kuwa huduma ya maji katika eneo hilo inapatikana kwa 40% hivyo wameweka mikakati ya kupandisha kiwango cha upatikanaji wa maji kwa kuanzisha mradi ambao wadau wake wakubwa ni serikali na shirika la maendeleo la uingereza (DFID).
Amemaliza kwa kuwataka wananchi kuwa wavumilivu wakati serikali inaendelea kupambana ili kutatua tatizo hilo.
Bw,John Sirikwa mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya maji katika mji mdogo wa Ngaramtoni amesema kuwa atajitahidi kufanikisha upatikanaji wa maji katika mji huo ili kutekeleza agizo la mgeni rasmi na kutatua changamoto zinazowakabili.
Aidha Bw,Aloyce Shayo amesema kuwa anaamini kuwa bdi itafanya vizuri kutokana na agizo la serikali itafanikiwa kufikia lengo.
Pia ametoan ushauri kwa bodi na kusema kuwa wajitume ilikufikia malengo na kuwataka wananchi kutoharibu vyanzo vya maji na kuvitunza kutokana na sheria ya utunzaji wa vyanzo vya maji.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh,Mashaka Mrisho Gambo,amewataka wananchi kuwa na vitambulisho vya Taifa mapema hii leo katika eneo la soko kuu mkoani Arusha.
Wakati akizindua rasmi zoezi la vitambulisho vya Taifa Mh,Gambo amesema kuwa lazima kila mtanzania awe na kitambulisho hicho kwani ndicho kitakachompelekea kufahamika kuwa yeye ni raia wa Tanzania.
Mh,Mashaka amehitimisha kwa kuwataka wananchi wote wa mkoa wa Arusha kuhakikisha wanapata vitambulisho hivyo kwani vitawasaidia kupunguza uhalifu katika jiji la Arusha
NA EUNICE ROBERT.
mkuu wa wilaya ya Arusha mh..FabianDaqaro amesema kuwa jiji la Arusha lipo salama kwa sasa lakini kuna wazushi wanaotumika na mataifa mengine ya nchi za nje kuanzisha maandamano hivyo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha wawakatae watu hao kama ukoma.
Ameendelea kusema kuwa mtu yoyote akiandamana itakula kwake hivyo amewataka wananchi hao kuwaacha wanaotaka kuandamana waandamane na familia zao.
hata hivyo bw.fabian ametoa onyo na kusema kuwa watu wanaotaka kuandaman waandamane wataona kitakachowatokea.
NA EUNICE ROBERT.
Gari la ILYANA linalofanya safari zake kutoka Arusha kuelekea mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mbeya limeharibika asubuhi ya leo na kusababisha abiria kukwama kwa zaidi ya saa 6 baada ya basi hilo walilokuwa wakisafiria kuharibika kila mita chache baada ya kutoka stendi kuu ya mabasi mkoani Arusha.
mmoja wa abiria wa gari hilo amesema kuwa mpaka sasa hawajapata ufumbuzi wa tatizo hilo wala gari lingine la kuwawezesha kuendelea na safari yao,hivyo ameomba vyombo vya ulinzi na usalama barabarani wajaribu kufuatilia chanzo cha tatizo hilo na kuwasaidia abiria kuweza kusafiri salama na kuendelea na shughuli zao nyingine.
lens pro media inaendelea kutafuta taarifa zaidi kuhusiana na jambo hili.
mwimbaji chipukizi wa nyimbo za injili miss moureen ametumbuiza katika kongamano la kinabii la kuvikwa uweza katika hotel ya corrido spring jijini Arusha.
ameimba wimbo wake wa yupo Mungu wakati waumini wakielekea kupokea neema ya utajiri kupitia mguu wa mtumishi wa Mungu nabii Erick Elisha ambaye alikufa kwa siku tano alipopata ajali ya ndege iliyosababisha kupoteza miguu yake miliwi na mkono wake mmoja .
miss Moureen amesema kuwa wimbo huu umewezeshwa na mwimbaji mwenzake Goodluck Gozbet ambaye alimsimamia kwanzia mwanzo mpaka mwisho hadi kukamilisha wimbo wake huo wa yupo Mungu.
wimbo wa miss Moureen yupo Mungu ni wimbo unaogusa maisha ya watu na kuleta faraja na amani ndani ya mioyo ya watu wa Mungu.
kongamano kubwa la kinabii na kuvikwa uweza limefanyika katika ukumbi wa corrido spring hotel ndani ya siku tatu huku baadhi ya watu wakifunguliwa na kupona magonjwa yao.
kongamano hilo la kinabii lililoongozwa na mtumishi wa Mungu nabii Erick Elisha liliambatana na waimbaji mbalimbali akiwemo mwimbaji wa nyimbo za injili Goodluck Gozbet na wengine wengi huku mahubiri yakitolewa na mtumishi wa Mungu Adam Haji.
katika kongamano hilo nabii Erick alitoa ushuhuda alivyo kufa kwa siku tano na kwenda kufanya matembezi mbinguni na kusema kuwa alipata ajali ya ndege iliyopelekea kupoteza miguu yake yote na mkono wake wa kulia .
hata hivyo aliongeza kuwa Mungu alimpa kibali cha kurudi duniani huku akiwa na neema ya utajiri aliyopewa na Mungu ndani ya mguu wake wa kushoto .
nabii Erick Elisha amehitimisha kwa kuwataka waumini kupokea neema hiyo ya utajiri aliyonayo kupitia mguu wake wa kushoto kwani watu wengi wamekuwa wakimuuliza siri ya utajiri wake na kumuomba awafundishe njia za kupata fedha ili kujikimu kimaisha.
wadau mbalimbali wa madini mkoani arusha wamelalamikia rpoti ya tarehe 12. 10.2015 ya madini iliyoeleza takwimu mbalimbali za uuzaji wa madini ikionyesha kudumaa kwa mapato yanayopatikana kwa uzalishaji nchini kutofutisha uuzaji wa asilimia kubwa nchi kama india na kenya
Hayo yamesemwa na thomas munis ambae ni makamu mwenyekiti TAMIDA kuiomba serikali kuboresha sekta hii ili mapato yaweze kupatikana bila kusahau ajira kwa vijana
''Taarifa hii imeizalilisha nchi kwani wazalishaji ndio wanapaswa kuingiza mapato makubwa kuliko wauzaj na suala kama hili nchi kama marekaniunaweza hata kunyongwa kwani hakuna mapato mazuri kwa serikali''alisema tomas
aidha bw.tomas amemaliza kwa kuishukuru serikali na kusema maboresho katika sekta hiyo kutaleta chachu ya uchumi na soko la kudumu ndani na nje ya nchi
waziri wa elimu prof joyce ndaichako ametoa agizo la kusimamisha kazi watumishi wote wa umma katika wizara yake walio na ajira zaidi ya moja hasa taasisi za elimu binafsi akiwa katika ziara yake mkoani arusha katika chuo kikuu cha mountmeru.
katika ziara yake waziri wa elimu amemfuta kazi felix sanyangwe aliyekuwa mdhibiti ubora wa shule ambapo mwaka 2015 alihamishiwa monduli lakini anaajira ya kudumu chuo kikuu cha mountmeru ambaye alijiuzulu na kutoroka alipopata taarifa ya ujio wa waziri huyo.
Prof ndalichako pia alisema kuwa kwa mujibu wa kanuni za utumishi kifungu cha f4 na f7 kinazuia mtumishi yoyote wa umma kuwa na ajira mbili na iwapo atabainika kuwa na ajira zaidi ya moja atapoteza ajira katika sekta ya utumishi wa umma.
Katika ziara yake pia amesisitiza kupanda kwa alama za ufaulu katika chuo hicho kwani hakuna chuo chochote kinacho toa alama ndogo za ufaulu kwa wanafunzi hapa nchini.
mratibu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA mkoa wa Arusha Bw.Samwel Marero.
Wafanyakazi na waajiriwa wa serikali na sekta binafsi wametakiwa kutumia sikukuu ya wafanyakazi ulimwenguni kwa kutafakari na kuboresha majukumu yao badala ya kuibua changamoto na mapungufu yanayojitokeza sehemu za kazi.
Rai hiyo imetolewa leo na mratibu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA mkoa wa Arusha Bw Samwel Marero Magero.
Bw.Marero amesisitiza wafanyakazi na waajiriwa wanapaswa kuwa kitu kimoja ili kuleta ufanisi kazini na kuwataka kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha sherehe hizo pamoja na kupata muafaka wa changamoto zao kwa ujumla.
kwa upande wake katibu wa chama cha wafanyakazi viwandani TWIKLE kanda ya kaskazini Bw.Hussein Ngowo wao kama waandaaji rasmi wa maadhimisho hayo wanahakikisha wanafanya uhamasishaji wa hali ya juu kufanikisha sherehe hizo.
Ameongeza kuwa tayari wameunda kamati ya maandalizi kwa kushirikiana na serikali kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha
Maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi mei mosi huazimishwa kila mwaka tarehe moja mwezi wa tano ambapo wafanyakazi ulimwenguni kote hutumia siku hiyo kutafakari na kutatua changamoto mbalimbali katika sehemu zao za kazi.