Theme images by MichaelJay. Powered by Blogger.

Visitors

Search This Blog



Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Youtube



Flickr Images

Like us on Facebook

Instagram

Facebook

Wednesday, March 28, 2018

HAKUNA USALAMA BILA MAJI NGARAMTON MKUU WA WILAYA YA MONDULi



NA EUNICE ROBERT

Mkuu wa wilya ya monduli ambaye pia ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa bodi mpya ya maji Ngaramtoni (NGAUWSA) Mh.Iddi Kimanta amezindua rasmi bodi mpya ya maji katika mji mdogo wa  Ngaramtoni mapema hii leo.



Akizungumza katika uzinduzi huo amesema kuwa bodi,viongozi na watumishi wengine wanapaswa kuelewa na kuona huduma zikoje kwani bima zinatoka kwenye vifaa vya maji.



Kwa upande wake Bw.Lembrice ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha amesema kuwa bodi ya maji NGAUWSA itakuwa na mamlaka ya kusimamia maji katika eneo la mamlaka ya mji mdogo Ngaramtoni kwa lengo la kutoa huduma bora ya maji safi na salama.



Bw.Lembrice ameendelea kusema kuwa wanategemea kuanzishwa kwa bodi hiyo kutasaidia maeneo ambayo hakuna maji waweze kupata kwa urahisi kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo halmashauri,wananchi,serikali kuu na wadau wengine wa maendeleo kuhusiana na swala zima la upatikanaji wa maji safi na salama.



Hivyo amehitimisha kwa kusema kuwa kuzinduliwa kwa bodi hii ni kwa mujibu wa sheria hivyo watekeleze wajibu waokwa kushirikiana na wadau wengine.



Aidha meneja wa mamlaka ya maji katika mji mdogo wa Ngaramtoni Bw,Claiison Kimaro amesema kuwa huduma ya maji katika eneo hilo inapatikana kwa 40% hivyo wameweka mikakati ya kupandisha kiwango cha upatikanaji wa maji kwa kuanzisha mradi ambao wadau wake wakubwa ni serikali na shirika la maendeleo la uingereza (DFID).



Amemaliza kwa kuwataka wananchi kuwa wavumilivu wakati serikali inaendelea  kupambana ili kutatua tatizo hilo.



Bw,John Sirikwa mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya maji katika mji mdogo wa Ngaramtoni amesema kuwa atajitahidi kufanikisha upatikanaji wa maji katika  mji huo ili kutekeleza agizo la mgeni rasmi na kutatua changamoto zinazowakabili.



Aidha Bw,Aloyce Shayo amesema kuwa anaamini kuwa bdi itafanya vizuri kutokana na agizo la serikali itafanikiwa kufikia lengo.



Pia ametoan ushauri kwa bodi na kusema kuwa wajitume ilikufikia malengo na kuwataka wananchi kutoharibu vyanzo vya maji na kuvitunza kutokana na sheria ya utunzaji wa vyanzo vya maji.

No comments:
Write comments

Interested for our works and services?
Get more of our update !