Sunday, March 25, 2018
ABIRIA WAKWAMA ZAIDI YA SAA 6 BAADA YA BASI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUHARIBIKA MKOANI ARUSHA
NA EUNICE ROBERT.
Gari la ILYANA linalofanya safari zake kutoka Arusha kuelekea mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mbeya limeharibika asubuhi ya leo na kusababisha abiria kukwama kwa zaidi ya saa 6 baada ya basi hilo walilokuwa wakisafiria kuharibika kila mita chache baada ya kutoka stendi kuu ya mabasi mkoani Arusha.
mmoja wa abiria wa gari hilo amesema kuwa mpaka sasa hawajapata ufumbuzi wa tatizo hilo wala gari lingine la kuwawezesha kuendelea na safari yao,hivyo ameomba vyombo vya ulinzi na usalama barabarani wajaribu kufuatilia chanzo cha tatizo hilo na kuwasaidia abiria kuweza kusafiri salama na kuendelea na shughuli zao nyingine.
lens pro media inaendelea kutafuta taarifa zaidi kuhusiana na jambo hili.
No comments:
Write comments