NA EUNICE ROBERT.
Pamoja na kuwepo kwa ushindani mkubwa kwa timu mbalimbali nchini lakini bado mkoa wa Arusha hauna timu ya ligi kuu.
Akizungumza na Lens Media Tv,Bw.Aloyce Sabuni ambaye ni mdau wa mpira wa miguu amesema kuwa misingi ya michezo mkoani Arusha imeanguka kwani mwanzo ilikuwa inajulikana kama Arusha ya vipaji lakini kwa sasa hata timu ya ligi kuu hakuna.
Ameongeza kwa kuomba uongozi wa TFF utazame jambo hili kwa uzito na kutafuta viongozi wa kusimamia na kupata timu ya ligi kuu ya mkoa.
Kwa upande wake Bw.Omary Mgaza ambaye ni mdau wa mpira amesema kuwa changamoto ni nyingi ikiwemo timu ya pepsi na timu ya madini lakini mpaka sasa timu hizi hazijulikani zilipo hivyo ameomba baadhi ya viongozi wa kubwa akiwemo mkuu wa mkoa na wa wilaya waweze kusimamia jambo hili.
Nae katibu wa chama cha mpira wa miguu Arusha Bw.Zakayo Mgema amesema kuwa miaka minne walikuwa kwenye kipindi cha mpito ndicho kilichosababisha kukosa timu ya ligi kuu lakini wamejipanga vizuri kwani timu ya Oljoro ipo daraja la kwanza hivyo kuwa na timu tatu daraja la kwanza ni rahisi kufika mbele kwa haraka.
No comments:
Write comments