NA EUNICE ROBERT
Pamoja na baadhi ya kaya kwenye mikoa mbalimbali kukumbwa na umaskini kutokana na kukosa fursa za kufanya biashara lakini bado mradi wa Tasaf umeendelea kusaidia kaya maskini mkoani Arusha.
Akizungumza na Lens Media Tv mkurugenzi mtendaji wa Tasaf Bw.Charles Wilson amesema kuwa mkoa wa Njombe na Arusha umepata bahati ya kuwa na miradi mingi kutokana na Tasaf ikiwemo mradi ya kuku pamoja na mbuzi.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa usimpe mtu samaki bali mpe ndoano akimaanisha kuwa hawawezi kutoa pesa kwa mtu bila kutoa mafunzo ya jinsi ya kuibua miradi mbalimbali na kusema kuwa mwaka huu watu wengi wameelimika na kuweza kuanzisha miradi mbalimbali ya kuwasaidia kujikimu kimaisha
Kwa upande wake msimamizi wa mradi wa Tasaf Bw.Elipokea Joseph amesema kuwa mradi huo mpya wa kuku waliouanzisha una wanufaika 75 ambao wamepata mifuko miwili ya chakula,chombo cha kunywea maji na chombo cha kuwawekea kuku chakula.
Nae mwanachama wa Tasaf Bi.Ndeshifose Elisamia amesema kuwa kipindi cha nyuma maisha yalikuwa magumu lakini kupitia mradi wa Tasaf wameweza kujikimu kimaisha na hata kuweza kuwapeleka watoto shule.
Afisa mtendaji wa Oldonyomasi Bw. Edward Joel amesema kuwa moja ya changamoto walizopata wakati wa kuandaa mradi huu ni muitikio wa wanachama kuwa mdogo kutokana na kukosa uelewa kuhusu mradi huo lakini wamefanikiwa kutatua changamoto hiyo na kwa sasa maendeleo yameonekana kutokana na mradi huo wa kuku.
No comments:
Write comments