WAZIRI WAAFYA MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO UMMY MWALIMU AKIWA
ANAZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA KUHAMASISHA UANZISHWAJI WA VIWANDA VYA DAWA
WAZIRI WA VIWANDA ,BIASHARA NA UWEKEZAJI MH.CHARLES MWIJAGE AKIWA ANAZUNGUMZA
NA EUNICE ROBERT
Serikali yawataka Wadau waUwekezaji nchini kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa ili kusaidia kupunguza gharama kubwa za matumizi zinazotokana na kununua, kusafirisha na kuhifadhi dawa zinazotoka nje ya nchi.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. UMMY MWALIMU katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini, kilichokutanisha wadau mbalimbali wa Uwekezaji katika Sekta ya Dawa, Vifaa na Vifaa tiba
Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imekuwa ikitumia zaidi ya trilion moja kununua dawa kutoka nje, hivyo kupitia uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini itasaidia kupunguza adha hiyo nchini kwa kiwango kikubwa.
Nae Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Mhe. Charles Mwijage amewataka wote wenye nia ya kuwekeza katika Ujenzi wa viwanda vya dawa, vifaa na vifaa tiba lazima wahakikishe wanashirikiana na taasisi za Utafiti zilizopo nchini ili kuangalia mahitaji na aina ya dawa zinazohitajika.
Aidha, Mhe. Charles Mwijage amehitimisha kwa kusema kuwa Uwekezaji na ujenzi wa Viwanda nchini utasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuchochea Maendeleo ya ukuaji wa Uchumi katika ngazi ya watu na taifa kwa ujumla.
No comments:
Write comments