NA EUNICE ROBERT
Mbunge wa Arusha mjini Mh.Godbles Lema amefikishwa mahakamani kwa kesi inayomkabili kwa tuhuma ya kuzungumza dhidi ya Rais John Pombe Magufuli ya mwaka 2016 mkoani Arusha.
Akizungumza na Lens Media Tv Mh Lema amesema kuwa kesi imesikilizwa na siku ya leo shahidi mwingine alitarajiwa kufika lakini hakimu amefuta kesi hiyo kupitia kifungu kidogo cha kwanza 225 kinachotoa mamlaka ya kujadiliana na jeshi la polisi kuhusu kesi hiyo.
Ameendelea kusema kuwa baada ya kupelekwa mahakamani hakimu mkazi sekei Arumeru amefuta kesi hiyo ambayo ilikuwa na mashahidi wa nne lakini bado upelelezi unaendelea.
Amehitimisha kwa kusema kuwa shtaka linalomkabili halina msingi wowote ,hivyo kesi iliyofutwa leo upelelezi wake haujakamilika.
No comments:
Write comments