NA EUNICE ROBERT
Pamoja na serikali kuendelea kutengeneza mikondo ya maji ili kuepusha mafuriko lakini bado baadhi ya maeneo mkoani Arusha yameendelea kukumbwa na adha ya mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa mtaa wa Lolovono mkoani humo wameeleza kile kilichotokea usiku wa kuamkia leo na kusema kuwa mvua zilizonyesha zimesababisha uharibifu mkubwa na kupoteza vitu vya ndani pamoja na kukosa mahali pa kulala kwani magodoro na vitanda vimechukuliwa na mafuriko hayo.
kwa upande wake Bi Dora John mhanga wa tukio hili amesema kuwa mafuriko hayo yamesababisha nguo za watoto wake kulowa na kupelekea kukosa nguo za kuwavalisha watoto wake pamoja na kukosa mahali pa kulala kwani nyumba zimebomoka na magodoro yamelowana.
Nae Bi Irene Izack shuhuda wa tukio hili amesema kuwa mafuriko hayo yameanza jana usiku muda wa saa nane ambapo walishtushwa na kelele zilizowafanya waweze kutafuta msaada wa haraka kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko hayo
wakazi hao wamehitimisha kwa kuiomba serikali iwasaidie kurekebisha mkondo wa maji kwani maji hayo yalizidi na kukosa njia ya kutokea hivyo yalitafuta njia iliyoko wazi ambapo kuna makazi ya watu na kusababisha uharibifu wa mali zao.
No comments:
Write comments