NA EUNICE ROBERT
Pamoja na serikali kuendelea kutilia mkazo wananchi kuhama kipindi hiki cha mvua maeneo ya bondeni na sehemu zenye mkondo wa maji lakini bado mvua hizo zimeendelea kuleta maafa mkoani Arusha.
Akizungumza na Lens Media Tv mkazi wa mlimani kikatiti Bi.Clementina Paulo amesema kuwa mvua kubwa imenyesha usiku wa kuamkia jana na kusababisha mafuriko ambayo yamebeba vyombo pamoja na magodoro.
Kwa upande wake mwalimu wa shule ya msingi kimara Bi.Eliminata Matoi amesema kuwa mvua hiyo iliyosababisha mafuriko imeleta maafa makubwa na kusababisha kushindwa kuendelea na shughuli za kila siku ikiwemo wanafunzi kwenda shuleni.
Nae mwenyekiti wa kitongoji cha mlimani Bw.Eliphasias Mtui amesema kuwa takribani kaya kumi na tano zimeharibiwa na mafuriko hayo pamoja na baadhi ya nyumba kuvunjwa ili kutoa maji yaliyoingia ndani hivyo ameiomba halmashauri kuongeza miundombinu ya kupitisha maji ili kuepuka matatizo hayo
Mwenyekiti wa kitongoji kambi ya mkaa Bw.Emmanuel Daniel amesema kuwa baadhi wa wakazi wa eneo hilo wamepata madhara makubwa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha watu kujifungia ndani na wanafunzi kushindwa kwenda shule.
No comments:
Write comments