NA EUNICE ROBERT
Katibu tawala mkoa wa Arusha Mh.Richard Kwitega amekabidhi mchango wa mifuko mia tatu ya sementi kwa ajili ya shughuli ya ujenzi wa Cathedral alioahidi Mh.Raisi John Pombe Joseph Magufuli siku ya tarehe nane katika sherehe za kumsimika Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Arusha Izack Amani.
Bw. Richard amesema kuwa amewasilisha mchango huo wa mifuko mia tatu ya sementi kwa niaba ya ikulu na kukabidhi kwa uongozi wa kanisa hilo kwa ajili ya kuwezesha kuendeleza ujenzi wa kanisa hilo lenye uwezo wa kuchukua takribani watu elfu tatu(3000)
Ameendelea kusema kuwa mchango wa rais Magufuli ni mkono mkubwa wa kuwezesha kukamilisha kanisa hilo na kuwaleta wakristo pamoja na kuwa mfano kwa viongozi wengine kuweza kujitoa kwa hali na mali kukamilisha ujenzi wa cathedral hiyo.
kwa upande wake katibu wa kamati ya ujenzi wa kanisa hilo Bw. Daniel Laizer amesema kuwa wamefurahishwa na kasi ya msaada huo na kumshukuru rais Magufuli kuonyesha mfano na pia wanaamini kuwa wengine watafwata kutoa michango yao.
Nae paroko wa parokia hiyo ya mtakatifu teresia wa mtoto Yesu Bw. Paul Malisa amesema kuwa rais Magufuli aliahidi kutoa mifuko mia tatu ya saruji akiwa kama kiongozi mkubwa wa nchi anayependa maendeleo lakini pia kama muumini wa kanisa katoliki nae ameshiriki kwa nafasi yake kama waumini wengine wanavyochangia
amehitimisha kwa kusema kuwa wanamuombea rais kuweza kufanikiwa kwenye uongozi wake Mungu amjalie afya njema aweze kuwahudumia watanzania wote bila ubaguzi.
No comments:
Write comments