NA EUNICE ROBERT
Meneja wa NSSF Bw.Frank Maduga amesema kuwa utaratibu walionao kwa sasa kwa wanachama wao wanakata asilimia kidogo ya mshahara kwa ajili ya mafao pale mwanachama anapostaafu.
Akizungumza na Lens Media Tv amesema kuwa wakikata mshahara kwa upande wa basic mwanachama akistaafu maisha yanakuwa tofauti na alivyokuwa kazini ikiwa na maana kuwa anapata mafao kidogo.
Ameendelea kusema kuwa anawahakikishia wanachama kuwa huduma hii itazidi kuwa bora na pia wanachama watoe ushirikiano kwa waajiri wao ili waweze kufikisha michango kwa wakati.
Kwa upande wake kaimu afisa kazi Arusha Bw.Wilyfredy Mdumi amesema kuwa waajiri waliofika kwenye semina hiyo wawe mabalozi wazuri kwa wenzao ili kuwahamasisha wanachama kuweza kutoa michango hiyo na kwa waajiri waweze kufikisha kwa wakati michango hiyo.
Pia ameongeza kuwa waajiri waandae semina nyingi kwa ajili ya wafanyakazi kwani wafanyakazi wengi hawana elimu kuhusu mfuko wa jamii,hivyo waajiri watoe elimu hiyo kwa wafanyakazi wao.
No comments:
Write comments