Theme images by MichaelJay. Powered by Blogger.

Visitors

Search This Blog



Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Youtube



Flickr Images

Like us on Facebook

Instagram

Facebook

Wednesday, April 11, 2018

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akifungua mkutano wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi uliofanyika mapema jana katika viwanja vya mbagala zakim jijini Dar-es-salaam.


  
Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimkaribisha mgeni rasmi makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.
                                                             


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hasssan akiangalia chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi baada ya kukabidhiwa na wataalamu wa masuala ya afya,wa kwanza kushoto ni waziri wa afya,maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto Mhe,Ummy Mwalimu.

Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu akipokea sindano ya chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kutoka kwa mtoa huduma za afya.kulia ni waziri wa afya maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe,Ummy Mwalimu.


Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu akipokea sindano ya chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kutoka kwa mtoa huduma za afya.kulia ni waziri wa afya maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe,Ummy Mwalimu.






   Picha ya pamoja ikionesha baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi waliohudhuria kumuunga mkono Mhe makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan wakatiwa uzinduzi wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.




NA EUNICE ROBERT
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan amezindua chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ili kutokomeza vifo vitokanavyo na magonjwa hapa nchini.

katika ufunguzi huo uliofanyika jana tarehe kumi mwezi wa nne jijini Dar-es-salaam makamu wa Rais Mhe,Samia amesema kuwa chanjo hiyo imewalenga wasichana wote wanaotimiza umri wa miaka 14 ili kuanza kujikinga mapema na ugonjwa huo.

"ili kupata kinga kamili,wasichana wanahitajika kupata dozi mbili ambapo dozi ya kwanza itatolewa muda wowote binti anapofikisha umri wa miaka 14 na dozi ya pili itatolewa muda wa miezi sita baada ya kupata dozi ya kwanza"alisema Mhe,Samia Suluhu.

Aidha Mhe,Samia amesema kuwa chanjo hiyo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi inatolewa bila ya malipo pamoja na uchunguzi wake kwani serikali imedhamiria kutokomeza tatizo hilo nchini.

"Niwaagize waganga wa mikoa na wilaya kuandaa kambi za wazi angalau mara tatu kwa mwaka ili kutoa huduma hiyo tena bila ya malipo kwa wanawake na wasichana wote mchini"alisisitiza makamu wa Rais Mhe,Samia Suluhu.
\
Mbali na hayo Mhe,Samia Suluhuamesema kuwa takribani wasichana laki sita kumi na sita elfu mia saba thelathini na nne wanatarajia kupata chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kwa mwaka 2018 na chanjo hiyo imethibitishwa na shirika la afya duniani (WHO).

Kwa upande wake waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe,Ummy Mwalimu amesema kuwa chanjo hii itakuwa ya saba kati ya chanjo ambazo zinatolewa kwa watoto ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali.

"Ukiacha chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi hapa nchini chanjo nyingine zinazotolewa ni ya kifua kikuu,polio,nimonia,kuharisha ama rota,surua na rubella,donda koo,kifaduro,homa ya ini,uti wa mgongo na pepopunda kwa watu wazima "alisema waziri Ummy.

Aidha waziri Ummy amesema kuwa serikali imefanikiwa kuweka maghala kuhifadhia chanjo katika mikoa yote nchini ambayo yana uwezo wa kuhifadhi chanjo kwa miezi sita bila ya kuharibika.

Kwa mujibu wa waziri Ummy amesema kuwa zawadi za fedha taslimu zitatolewa kwa mikoa mitatu itakayofanya vizuri katika utoaji wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi hapa nchini.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam Mhe,Paul Makonda amesema kuwa wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kwenda kupata vipimo na chanjo za kukinga saratani pindi wanapogundulika wana magonjwa hayo

"Natoa rai kwa wananchi mliojitokeza hapa kuwapeleka watoto wenu,wake zenu na wanawake wote hususani wasichana wenye umri wa miaka 14 kwenda kupata chanjo hii na mkifika majimbani kwenu muwakumbushe watu wenu wa karibu kushiriki katika upataji wa chanjo hii"alisema Mhe,Makonda.


No comments:
Write comments

Interested for our works and services?
Get more of our update !