NA EUNICE ROBERT
Kismaty Media imefanya tamasha tarehe 28/4/2018 la kuibua vipaji vichanga vya wasanii mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali mkoani Arusha.
Akizungumza na Lens Media Tv mkurugenzi wa Kismaty Bi.Mary Mollel amesema kuwa dhumuni la kuanzisha tamasha hilo ni kukuza vipaji kwani kuna watu wenye vipaji mbalimbali lakini wamelenga zaidi kwenye upande wa watu wenye vipaji vya kuimba bongo fleva.
Pia ameendelea kusema kuwa matarajio yao ni kuibua vipaji vilivyojificha mkoani Arusha na kwa mshindi wa kwanza atapata zawadi ya gari,mshindi wa pili atapata zawadi ya bajaji na wa tatu atapata zawadi ya pikipiki.
Ameendelea kusema kuwa awamu ya kwanza watachuja watu hamsini,awamu ya pili watachuja mpaka kufikia watu kumi ambapo fainali inatarajiwa kuwa tarehe 19/5/2018.
Bi Mary ameongeza kuwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapata zawadi lakini kwa waliosalia watafanyiwa video bure na mambo mengine yahusuyo muziki.
Amehitimisha kwa kusema kuwa mashindano haya yameanza rasmi mkoani Arusha na wana malengo ya kuendeleza mikoa mbalimbali ikiwemo Moshi,Tanga na Dar-es-salaam.
No comments:
Write comments