NA EUNICE ROBERT
Pamoja na watu kuendelea kujihadhari na mvua zinazoendelea kunyesha nchini lakini bado kuna baadhi ya maeneo yameendelea kuathirika kutokana na mafuriko mkoani Arusha.
Akizungumza na Lens Media Tv Bw.Ismail Abraham ambaye ni mkazi wa Oldonyomasi amesema kuwa tatizo kubwa linalowasumbua wakazi wa eneo hilo ni barabara kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha .
Bw.Ismail amehitimisha kwa kuiomba serikali kuwawekea vifusi kwenye barabara hiyo ili kuweza kuwasaidia wakazi wa eneo hilo kuweza kupita bila kuzama na kuendelea na shughuli zao za kujenga Taifa.
kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Oldonyomasi Bw.Patrick Massawe amesema kuwa kutokana na matope hayo kumekuwa vigumu kupita kwa magari,watembea kwa miguu na hata bodaboda.
Ameendelea kusema kuwa bodaboda wajitolee kufukia barabara hiyo ili kuweza kupita na kuendelea na shughuli zao za kujitafutia riziki
Bw.Patrick amehitimisha kwa kutoa wito kwa wakulima wa eneo hilo kuweka kingo kwenye mashamba yao ili kuzuia mmomonyoko wa udongo unaosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha lengo likiwa ni kulinda mazao yasiharibiwe na maji yatokanayo na mvua.
No comments:
Write comments