NA EUNICE ROBERT
Katika kuelekea sikukuu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar,jeshi la polisi mkoa wa Arusha limejipanga vizuri kuhakikisha sikukuu hiyo inafanyika kwa amani.
Akizungumza na Lens Media Tv kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoni Arusha BwYusuph Ilembo amesema kuwa wanafunzi wanapaswa kusoma na kuachana na mambo ambayo yanaharibu malengo yao hivyo amewataka watii sheria za nchi ili kuepuka matatizo.
Ameongeza kwa kusema kuwa wafanyabiashara na wakulima wanapaswa kufanya shughuli za kuleta maendeleo kwenye taifa na kuachana na kufanya mambo ya kushinikizwa,hivyo watakaovunja sheria siku ya muungano watajutia.
No comments:
Write comments