NA EUNICE ROBERT
Bwana shamba wa ECO Bw.Biniventure ameeleza adhari za jani lijulikanalo kwa jina la gugu karoti ambalo ni hatari kwa maisha ya binadamu na wanyama mkoani Arusha.
Akizungumza na Lens Media Tv Bw.Biniventure amesema kuwa wamefanya uhamasishaji wa kuangamiza jani hilo kwani limeenea zaidi mkoa wa Arusha na linaota maeneo ya barabarani,majumbani na mashambani.
Pia ameongeza kuwa jani hili limeua baadhi ya wanyama kata ya Terati na eneo la Tengeru,hivyo wamefanya semina ili kuelimisha jamii kwani wanafunzi wamekuwa wakitumia kama mafagio jambo ambalo linapelekea kudhurika kwenye mikono yao.
Hata hivyo ametoa angalizo kwa jamii kuwa jani hili ni hatari hivyo lishikwe kwa kutumia gloves ili lisishike eneo la mwili kwani ni hatari.
Kwa upande wake mfanyakazi wa ECO Bw.Daudi Lomayani amesema kuwa wamefanya semina na wageni kutoka jimbo la Florida Marekani kwa ajili ya kuwasaidia wananchi na jamii kwa ujumla ili wasiendelee kuathirika na jani hilo aina ya gugu karoti
No comments:
Write comments