NA EUNICE ROBERT
Wakazi wa Ngaramtoni mtaa wa Olorieni mkoani Arusha wameandamana kuomba kibali cha kutengeneza barabara ili kutatua changamoto zinazowakabili kutokana na mafuriko yanayosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha
akizungumza na Lens Media Tv mmoja wa wakazi wa mtaa huo Bi.Grace Zakayo amesema kuwa mafuriko hayo yameharibu barabara na kupelekea kuelekea katika ofisi za serikali ya mtaa huo lakini hawakupata ushirikiano hali inayopelekea watu kupata shida na wagonjwa kukosa huduma ya haraka pale wanapougua nyakati za usiku
Nae mwenyekiti wa bodi ya shule ya Mringa Bw.Noel Abraham amesema kuwa kipindi hiki cha mvua mafuriko yamekithiri hali inayopelekea watoto kushindwa kwenda shule na kusababisha watoto hao kuogelea ndani ya maji hayo kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa maisha yao.
ameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa eneo hilo lililofunguliwa barabara litawasaidia watoto na wakazi wa eneo hilo kufanya shughuli zao bila shida pia ameiomba serikali kuwatengenezea miundombinu bora ili kuepukana na mafuriko katika kipindi hiki cha mvua.
kwa upande wake Bw.Zakayo Kivuyo amesema kuwa wamefarijika na kutengenezewa barabara hiyo kwani barabara waliyokuwa wanatumia ilikuwa imeshaharibiwa na mafuriko lakini kwa sasa kero hiyo imewaepuka baada ya kupata kibali cha serikali ya mtaa huo cha kurekebishiwa barabara hiyo.
Aidha Bw.John Nguvula amesema kuwa wamejitolea kutengeneza barabara hiyo kwani ilikuwa inahatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo hasa watoto wanaoenda shule,hivyo ameishukuru serikali ya mtaa wa Olorieni kuwapa kibali cha kutengeneza barabara hiyo mpaka kufanikiwa.
No comments:
Write comments