NA EUNICE ROBERT
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kufungua kituo cha polisi cha kisasa cha kwanza hapa nchini siku ya jumamosi kitakachotoa huduma kwa watalii na wanadiplomasia jijini Arusha.
Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa pamoja na mambo mengine raisi atazindua nyumba za askari zilizopo kituo cha polisi cha kati.
Bw.Charles ameendelea kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na maonyesho ya utendaji kazi wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha yatakayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid hivyo ametoa wito kwa wananchi na wakazi wa Arusha kufika bila kukosa ili kushuhudia uimara wa jeshi la polisi.
Aidha ameongeza kuwa nyumba za polisi zimekamilika na mara baada ya kufunguliwa zitaanza kutumika pia ameendelea kusema kuwa kutafanyika ufunguzi wa vituo viwili vya polisi kwani hapa nchini Tanzania hakujawahi kuwa na kituo cha kidiplomasia hivyo amesema kuwa jeshi la polisi limeamua kufungua kituo kikubwa cha kisasa kitakachofunguliwa na Mh.raisi John Pombe Magufuli.
Amehitimisha kwa kusema kuwa kituo kingine cha kisasa cha daraja la kati ambacho kitatoa huduma kata ya Murieti kwa Morombo kitafunguliwa siku hiyo hivyo amewataka wananchi kuhudhuria siku hiyo kwa ajili ya kushuhudia ufunguzi wa nyumba hizo na utendaji kazi wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha.
No comments:
Write comments