Theme images by MichaelJay. Powered by Blogger.

Visitors

Search This Blog



Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Youtube



Flickr Images

Like us on Facebook

Instagram

Facebook

Sunday, April 29, 2018

zawadi ya gari kutoka kismaty media kushindaniwa mkoani Arusha



NA EUNICE ROBERT

Kismaty Media imefanya tamasha tarehe 28/4/2018 la kuibua vipaji vichanga vya wasanii mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali mkoani Arusha.

Akizungumza na Lens Media Tv mkurugenzi wa Kismaty Bi.Mary Mollel amesema kuwa dhumuni la kuanzisha tamasha hilo ni kukuza vipaji kwani kuna watu wenye vipaji mbalimbali lakini wamelenga zaidi kwenye upande wa watu wenye vipaji vya kuimba bongo fleva.

Pia ameendelea kusema kuwa matarajio yao ni kuibua vipaji vilivyojificha mkoani Arusha na kwa mshindi wa kwanza atapata zawadi ya gari,mshindi wa pili atapata zawadi ya bajaji na wa tatu atapata zawadi ya pikipiki.

Ameendelea kusema kuwa awamu ya kwanza watachuja watu hamsini,awamu ya pili watachuja mpaka kufikia watu kumi ambapo fainali inatarajiwa kuwa tarehe 19/5/2018.

Bi Mary ameongeza kuwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapata zawadi lakini kwa waliosalia watafanyiwa video bure na mambo mengine yahusuyo muziki.

Amehitimisha kwa kusema kuwa mashindano haya yameanza rasmi mkoani Arusha na wana malengo ya kuendeleza mikoa mbalimbali ikiwemo Moshi,Tanga na Dar-es-salaam.

Friday, April 27, 2018

misharaa mitatu kwa kila mwanachama-NSSF



NA EUNICE ROBERT

Meneja wa NSSF Bw.Frank Maduga amesema kuwa utaratibu walionao kwa sasa kwa wanachama wao  wanakata asilimia kidogo ya mshahara kwa ajili ya mafao pale mwanachama anapostaafu.

Akizungumza na Lens Media Tv amesema kuwa wakikata mshahara kwa upande wa basic mwanachama akistaafu maisha yanakuwa tofauti na alivyokuwa kazini ikiwa na maana kuwa anapata mafao kidogo.

Ameendelea kusema kuwa anawahakikishia wanachama kuwa huduma hii itazidi kuwa bora na pia wanachama watoe ushirikiano kwa waajiri wao ili waweze kufikisha michango kwa wakati.

Kwa upande wake kaimu afisa kazi Arusha Bw.Wilyfredy Mdumi amesema kuwa waajiri waliofika kwenye semina hiyo wawe mabalozi wazuri kwa wenzao ili kuwahamasisha wanachama kuweza kutoa michango hiyo na kwa waajiri waweze kufikisha kwa wakati michango hiyo.

Pia ameongeza kuwa waajiri waandae semina nyingi kwa ajili ya wafanyakazi kwani wafanyakazi wengi hawana elimu kuhusu mfuko wa jamii,hivyo waajiri watoe elimu hiyo kwa wafanyakazi wao.




Kesi ya lema



NA EUNICE ROBERT

Mbunge wa Arusha mjini Mh.Godbles Lema amefikishwa mahakamani kwa kesi inayomkabili kwa tuhuma ya kuzungumza dhidi ya Rais John Pombe Magufuli ya mwaka 2016 mkoani Arusha.

Akizungumza na Lens Media Tv Mh Lema amesema kuwa kesi imesikilizwa na siku ya leo shahidi mwingine alitarajiwa kufika lakini hakimu amefuta kesi hiyo kupitia kifungu kidogo cha kwanza 225 kinachotoa mamlaka ya  kujadiliana na jeshi la polisi kuhusu kesi hiyo.

Ameendelea kusema kuwa baada ya kupelekwa mahakamani hakimu mkazi sekei Arumeru amefuta kesi hiyo ambayo ilikuwa na mashahidi wa nne lakini bado upelelezi unaendelea.

Amehitimisha kwa kusema kuwa  shtaka linalomkabili  halina msingi wowote ,hivyo kesi iliyofutwa leo upelelezi wake haujakamilika.

wafanyabiashara waadilifu kupitisha mizigo bandarini bila usumbufu.



NA EUNICE ROBERT

Pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia bandari kupitisha mizigo yao kuwa wakaidi wa kutokulipa ushuru lakini bado serikali imeendelea kufanikiwa kudhibiti hali hiyo.

Akizungumza na Lens Media Tv kaimu kamishna wa forodha na ushuru wa bidhaa Tanzania Mh.Ben Usaje amesema kuwa mradi wa kwanza waliobuni ni single custom territory ili kupunguza gharama na muda unaotumika kusafirisha mizigo kutoka badari ya mombasa na Dar-es-salaam kwenda kwenye nchi zisizona bandari.

Bw.Ben ameendelea kusema kuwa mradi huo unasaidia nchi husika ambayo mzigo unaenda kuweza kuandika ripoti ya mzigo huo kabla haujafika ikiwa na maana ya kulinda bidhaa za viwanda vilivyopo nchini.

Ameongeza kuwa wameanzisha mfumo ambao unasaidia kuwafanya wafanyabiashara kusema ukweli wa bidhaa zao bila kudanganya na kuepusha usumbufu wa kukagua na kufanya utaratibu wa kukagua mzigo kama ni wenyewe.

Amehitimisha kwa kusema kuwa bado mawakala wa forodha hawana ruhusa ya kuangalia bei na bidhaa kutoka nchi zingine ili waweze kuagiza

Wednesday, April 25, 2018

Polisi arusha waonya dhidi ya wanaotaka kuandamana tar 26/04



NA EUNICE ROBERT

Katika kuelekea sikukuu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar,jeshi la polisi mkoa wa Arusha limejipanga vizuri kuhakikisha sikukuu hiyo inafanyika kwa amani.

Akizungumza na Lens Media Tv kaimu  kamanda wa jeshi la polisi mkoni Arusha BwYusuph Ilembo amesema kuwa wanafunzi wanapaswa kusoma na kuachana na mambo ambayo yanaharibu malengo yao hivyo amewataka watii sheria za nchi ili kuepuka matatizo.

Ameongeza kwa kusema kuwa wafanyabiashara na wakulima wanapaswa kufanya shughuli za kuleta maendeleo kwenye taifa na kuachana na kufanya mambo ya kushinikizwa,hivyo watakaovunja sheria siku ya muungano watajutia.




Tuesday, April 24, 2018

UKOMBOZI WA TASAF KWA KAYA MASKINI MKOANI ARUSHA.



NA EUNICE ROBERT

Pamoja na baadhi ya kaya kwenye mikoa mbalimbali kukumbwa na umaskini kutokana na kukosa fursa za kufanya biashara lakini bado mradi wa Tasaf umeendelea kusaidia kaya maskini mkoani Arusha.

Akizungumza na Lens Media Tv mkurugenzi mtendaji wa Tasaf Bw.Charles Wilson amesema kuwa mkoa wa Njombe na Arusha umepata bahati ya kuwa na miradi mingi kutokana na Tasaf ikiwemo mradi ya kuku pamoja na mbuzi.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa usimpe mtu samaki bali mpe ndoano akimaanisha kuwa hawawezi kutoa pesa kwa mtu bila kutoa mafunzo ya jinsi ya kuibua miradi mbalimbali na kusema kuwa mwaka huu watu wengi wameelimika na kuweza kuanzisha miradi mbalimbali ya kuwasaidia kujikimu kimaisha

Kwa upande wake msimamizi wa mradi wa Tasaf Bw.Elipokea Joseph amesema kuwa mradi huo mpya wa kuku waliouanzisha una wanufaika  75 ambao wamepata mifuko miwili ya chakula,chombo cha kunywea maji  na chombo cha kuwawekea kuku chakula.

Nae mwanachama wa Tasaf Bi.Ndeshifose Elisamia amesema kuwa kipindi cha nyuma maisha yalikuwa magumu lakini kupitia mradi wa Tasaf wameweza kujikimu kimaisha na hata kuweza kuwapeleka watoto shule.

Afisa mtendaji wa Oldonyomasi Bw. Edward Joel amesema kuwa moja ya changamoto walizopata wakati wa kuandaa mradi huu ni muitikio wa wanachama kuwa mdogo kutokana na kukosa uelewa kuhusu mradi huo lakini wamefanikiwa kutatua changamoto hiyo na kwa sasa maendeleo yameonekana kutokana na mradi huo wa kuku.


semina ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa waandishi wa habari mkoani Arusha



NA EUNICE ROBERT.

Semina kuhusu chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi imetolewa kwa waandishi wa habari mkoani Arusha  kwani wao ndio nguzo kubwa ya kuunganisha wataalamu wa afya na jamii lengo likiwa ni kuelimisha jamii.

Akizungumza na Lens Media Tv mganga mkuu Arusha Dkt.Onanji Vivian amesema kuwa wamefanya semina hiyo kwa waandishi wa habari  kwa sababu itakuwa rahisi kwa jamii kupata elimu hii ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.

Hata hivyo ameendelea kusema kuwa wao kama timu ya uwezeshaji wa huduma za afya  mkoa wa Arusha na wataalamu wa afya duniani WHO wamefanya semina hiyo kwa waandishi wa habari ili taarifa watakazoziandika na uhamasishaji watakaoufanya ukawe na ukweli ndani yake ili jamii ifahamu kuwa chanjo hii ni salama.

Aidha amesema kuwa chanjo hii itatolewa kwa watoto wenye miaka kumi na nne na zoezi hilo litazinduliwa rasmi tarehe 25/4/2018.

Kwa upande wake daktari mwandamizi tamisemi Dkt.Bonifas Nguvun amesema kuwa chanjo hiyo itatolewa kwa watoto kwanzia miaka tisa mpaka kumi na nne kwani chanjo hii hailengi walioanza kujamiiana badala yake inawalenga wale ambao hawajawahi kujamiiana.

Pia ameongeza kuwa chanjo hii haitahusika kwa watu wazima kwani haitoweza kufanya kazi ipasavyo na kusema kuwa inapaswa mtu kupata chanjo kabla ya kuanza kujamiiana.

Nae Bi Vero Mheta ambae ni mwandishi wa habari amesema kuwa wanahabari wako tayari kutoa elimu kwa jamii kuhusu chanjo hii lakini pia ametoa wito kwa wasichana wenye umri wa miaka tisa mpaka kumi na nne kujitokeza kupata chanjo hiyo kwani ugonjwa huo umepoteza wasichana wengi na hata vijana.

Saturday, April 21, 2018

Arusha wanapenda pombe kuliko michezo/ukosefu wa timu ya ligi kuu Arusha



NA EUNICE ROBERT.

Pamoja na kuwepo kwa ushindani mkubwa kwa timu mbalimbali nchini lakini bado mkoa wa Arusha hauna timu ya ligi kuu.

Akizungumza na Lens Media Tv,Bw.Aloyce Sabuni ambaye ni mdau wa mpira wa miguu amesema kuwa misingi ya michezo mkoani Arusha imeanguka kwani mwanzo ilikuwa inajulikana kama Arusha ya vipaji lakini kwa sasa hata timu ya ligi kuu hakuna.

Ameongeza kwa kuomba uongozi wa TFF utazame jambo hili kwa uzito na kutafuta viongozi wa kusimamia na kupata timu ya ligi kuu ya mkoa.

Kwa upande wake Bw.Omary Mgaza ambaye ni mdau wa mpira amesema kuwa changamoto ni nyingi ikiwemo timu ya pepsi na timu ya madini lakini mpaka sasa timu hizi hazijulikani zilipo hivyo ameomba baadhi ya viongozi wa kubwa akiwemo mkuu wa mkoa na wa wilaya waweze kusimamia jambo hili.

Nae katibu wa chama cha mpira wa miguu Arusha Bw.Zakayo Mgema amesema kuwa miaka minne walikuwa kwenye  kipindi cha mpito ndicho kilichosababisha kukosa timu ya ligi kuu lakini wamejipanga vizuri  kwani timu ya Oljoro ipo daraja la kwanza hivyo kuwa na timu tatu daraja la kwanza ni rahisi kufika mbele kwa haraka.


VIDEO KALI ILIYOFANYIKA CALFONIA.

Msanii kutoka Arusha Harryvice  ametoa nyimbo yake mpya,ngoma inaitwa pamela na amefanyanya na mtu mzima Magga v kutoka pande hizi hizi za Arusha.

Video hii imefanyika Kalizone ikiwa imesimamiwa kwa uzuri kabisa na mtu mzima director first born na kutengenezwa na producer Fex.

Ngoma imegharimu zaidi ya million moja kwanzia maandalizi mpaka kukamilika kwake na ni bonge moja la video

Cha kufanya ni kuitazama pamela ili kutoa support kwa msanii Harryvice pamoja  na Magga V.
KAMA HUJAPATA NAFASI YA KUIONA VIDEO YA PAMELA.ITAZAME.

Friday, April 20, 2018

Mvua zazid kusababisha maafa jijin Arusha....



NA EUNICE ROBERT

Pamoja na serikali kuendelea kutilia mkazo wananchi kuhama kipindi hiki cha mvua  maeneo ya bondeni na sehemu zenye mkondo wa maji lakini bado mvua hizo zimeendelea kuleta maafa mkoani Arusha.

Akizungumza na Lens Media Tv mkazi wa mlimani kikatiti Bi.Clementina Paulo amesema kuwa mvua kubwa imenyesha usiku wa kuamkia jana na kusababisha mafuriko ambayo yamebeba vyombo pamoja na magodoro.

Kwa upande wake mwalimu wa shule ya msingi kimara Bi.Eliminata Matoi amesema kuwa mvua hiyo iliyosababisha mafuriko imeleta maafa makubwa na kusababisha kushindwa kuendelea na shughuli za kila siku ikiwemo wanafunzi kwenda shuleni.

Nae mwenyekiti wa kitongoji cha mlimani Bw.Eliphasias Mtui amesema kuwa takribani kaya kumi na tano zimeharibiwa na mafuriko hayo pamoja na baadhi ya nyumba kuvunjwa ili kutoa maji yaliyoingia ndani hivyo ameiomba halmashauri kuongeza miundombinu ya kupitisha maji ili kuepuka matatizo  hayo

Mwenyekiti wa kitongoji kambi ya mkaa Bw.Emmanuel Daniel amesema kuwa baadhi wa wakazi wa eneo hilo wamepata madhara makubwa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha watu kujifungia ndani na wanafunzi kushindwa kwenda shule.

Thursday, April 19, 2018

VIDEO YAGHARIMU MAMILIONI YA PESA



Msanii kutoka Moshi Kilimanjaro,Tivah, ametoa nyimbo mpya wiki mbili zilizopita,nyimbo  inaitwa Kokodosa amefanya na Uraniium na kumshirikisha Single Sally.

video hii imechukua wiki moja kukamilika na imefanyika Moshi kwenye pub ya black diamond na aliyesimamia show nzima namaanisha director wa video hii ni mtu mzima Hasanally ambaye anakuja kwa kasi sana mkoani Kilimanjaro.

Mikakati ya project mpya ya kutoa ngoma nyingine,new hit song imeshaanza na very soon mashabiki wa msanii mwanadada Tivah pamoja na Uranium wakae tayari kwa hit song nyingine mapema sanaa.

kwa upande wa cost amesimamia mtu mzima Uranium pamoja na Tivah bila kumsahau Single Sally na kusababisha mzigo kufika kiuhalali bila shida yoyote.

kutokana na changamoto za madancer au wachezaji kwenye ngoma hii kuchelewa kufika location,lakini mtu mzima director Hasanally aliitendea haki video huku mkali mwenyewe producer Not  akifanya yake kwa ustadi mkubwa.

mafanikio waliyoyapata tangu watoe video yao hii ya KOKODOSA wiki mbili zilizopita wamefanikiwa kufanya show tatu ambazo wamefanya vizuri na kujipatia kipato au shavu.

Big up sanaaa kwa producer Not kutoka high level studio akishirikiana na iyogo beat kwa kutengeneza kazi nzuri ambayo inaonekana hapo juu ikiwa na high quality.

video ni mpya na ni kali cha kufanya ni kuitazama video hii ili kuwapa support wasanii hawa Tivah & Uranium ft Single Sally ili waweze kufanya vizuri zaidi na zaidi.

Tuesday, April 17, 2018

Wanawake waaswa kujifunza matumiz sahihi ya mitandao na kujifunza zaid k...



NA EUNICE ROBERT

Wanawake kote nchini wameaswa kujifunza matumizi sahihi ya mitandao ili kukua kiteknolojia kwani kuna umuhimu wa kutumia teknolojia kwenye karne hii ya ishirini na moja.

Akizungumza na Lens Media Tv mkurugenzi wa Zaina Foundation Bi.Zainab amesema kuwa wasichana na wanawake wamekuwa nyuma sana kwenye matumizi ya teknolojia na pia hawapewi nafasi ya kuweza kujifunza ili kujua mambo mbalimbali yanayohusu  teknolojia.

Ameongeza kwa kusema kuwa endapo watapata uelewa wa jinsi ya kutumia teknolojia wanaweza kutumia kwa kusoma na kwenye maswala ya afya.

Ameendelea kusema kuwa wanatarajia kila kitu kitumike kwa kuzingatia teknolojia inavyokuwa hivyo wamefanya semina na wanawake ili kuwapa elimu hiyo ya kutumia teknolojia.

Kwa upande wake Bw.Frank Nduguru ambaye ni mmoja wa washiriki amesema kuwa wamejifunza mambo mengi kuhusu Cyber Crimes na kutumia teknolojia kwa matumizi sahihi na sio kutuma picha zisizo na maadili kwa jamii ya kitanzania.

Nae Bi,Magdalena Mhina amesema kuwa wanatarajia kuwa wasichana watajilinda kuhusiana na maswala ya uzazi ili kuweza kufikia malengo yao kwa kutumia teknolojia kwa usahihi


Mvua zazid kuleta maafa jijin Arusha



NA EUNICE ROBERT

Pamoja na watu kuendelea kujihadhari na mvua zinazoendelea kunyesha nchini lakini bado kuna baadhi ya maeneo yameendelea kuathirika kutokana na mafuriko mkoani Arusha.

Akizungumza na Lens Media Tv Bw.Ismail Abraham ambaye ni mkazi wa Oldonyomasi amesema kuwa tatizo kubwa linalowasumbua wakazi wa eneo hilo ni barabara kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha .

 Bw.Ismail amehitimisha kwa kuiomba serikali kuwawekea vifusi kwenye barabara hiyo ili kuweza kuwasaidia wakazi wa eneo hilo kuweza kupita bila kuzama na kuendelea na shughuli zao za kujenga Taifa.

kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Oldonyomasi Bw.Patrick Massawe amesema kuwa  kutokana na matope hayo kumekuwa vigumu kupita kwa magari,watembea kwa miguu na hata bodaboda.

Ameendelea kusema kuwa bodaboda wajitolee kufukia barabara  hiyo ili kuweza kupita na kuendelea na shughuli zao za kujitafutia riziki

Bw.Patrick amehitimisha kwa kutoa wito kwa wakulima wa eneo hilo kuweka kingo kwenye mashamba yao ili kuzuia mmomonyoko wa udongo unaosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha lengo likiwa ni kulinda mazao yasiharibiwe na maji yatokanayo na mvua.




Saturday, April 14, 2018

JANI HATARI KWA MAISHA YA BINADAMU NA WANYAMA



NA EUNICE ROBERT

Bwana shamba wa ECO Bw.Biniventure ameeleza adhari za jani lijulikanalo kwa jina la gugu karoti ambalo ni hatari kwa maisha ya binadamu na wanyama mkoani Arusha.

Akizungumza na Lens Media Tv Bw.Biniventure amesema kuwa wamefanya uhamasishaji wa kuangamiza jani hilo kwani limeenea zaidi mkoa wa Arusha na  linaota maeneo ya barabarani,majumbani na mashambani.

Pia ameongeza kuwa jani hili limeua baadhi ya wanyama kata ya Terati na eneo la Tengeru,hivyo wamefanya semina  ili  kuelimisha jamii kwani wanafunzi wamekuwa wakitumia kama mafagio jambo ambalo linapelekea kudhurika kwenye mikono yao.

Hata hivyo ametoa angalizo kwa jamii kuwa jani hili ni hatari hivyo lishikwe kwa kutumia gloves ili lisishike eneo la mwili kwani ni hatari.

Kwa upande wake mfanyakazi wa ECO Bw.Daudi Lomayani amesema kuwa wamefanya semina na wageni kutoka jimbo la Florida Marekani kwa ajili ya kuwasaidia wananchi na jamii kwa ujumla ili wasiendelee kuathirika na jani hilo aina ya gugu karoti

Friday, April 13, 2018

UKOSEFU WA KIWANJA CHA MPIRA WA KIKAPU JIJINI ARUSHA..



NA EUNICE ROBERT

Mjumbe wa chama cha mpira wa kikapu Arusha Bw.Bariki Kilimba ameeleza adha wanayoipata kutokana na  ukosefu wa kiwanja cha kufanyia mazoezi na kuchezea mpira wa kikapu jijini Arusha.

Akizungumza na Lens Media Tv Bw.Bariki amesema kuwa chama cha mpira wa kikapu Arusha kiliwapeleka baadhi ya wadau kwenda kusoma Uganda na Nairobi nia ikiwa ni kuwafundisha watoto na vijana.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa ukosefu wa kiwanja hicho cha mpira wa kikapu kunawaathiri kwa kiasi kikubwa kwani walikuwa wakitegemea kiwanja cha Soweto lakini kwa sasa wamezuiliwa kwa muda kwa ajili ya usalama zaidi kwani  kuna makazi ya watu katika eneo hilo.

Aidha ameendelea kusema wameshindwa kufanya ligi ya mkoa ambapo walitegemea kupeleka timu ya mkoa kushindana jijini Dar-es-salaam lakini imeshindikana kutokana na ukosefu wa kiwanja cha kufanya mazoezi

Amehitimisha kwa kusema kuwa chama cha mpira wa kikapu hakihitaji fedha kutoka serikalini kwa sababu wana wafadhili hivyo wameiomba serikali kuwapatia eneo la wazi kwa lengo la kujenga kiwanja cha mpira wa kikapu ili kukuza vipaji vya watoto na vijana.


Wednesday, April 11, 2018

Wananchi waandamana kwenda kuomba kibal cha kujitengenezea barabara Nga...





NA EUNICE ROBERT

Wakazi wa Ngaramtoni mtaa wa Olorieni mkoani Arusha wameandamana kuomba kibali cha kutengeneza barabara ili kutatua changamoto zinazowakabili kutokana na mafuriko yanayosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha

akizungumza na Lens Media Tv mmoja wa wakazi wa mtaa huo Bi.Grace Zakayo amesema kuwa mafuriko hayo yameharibu barabara na kupelekea kuelekea katika ofisi za  serikali ya mtaa huo lakini hawakupata ushirikiano hali inayopelekea watu kupata shida na wagonjwa kukosa huduma ya haraka pale wanapougua nyakati za usiku

Nae mwenyekiti wa bodi ya shule ya Mringa Bw.Noel Abraham amesema kuwa kipindi hiki cha mvua mafuriko yamekithiri hali inayopelekea watoto kushindwa kwenda shule na kusababisha watoto hao kuogelea ndani ya maji hayo kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa maisha yao.

ameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa eneo hilo lililofunguliwa barabara litawasaidia watoto na wakazi wa eneo hilo kufanya shughuli zao bila shida pia ameiomba serikali kuwatengenezea miundombinu bora ili kuepukana na mafuriko katika kipindi hiki cha mvua.

kwa upande wake Bw.Zakayo Kivuyo amesema kuwa wamefarijika na kutengenezewa barabara hiyo kwani barabara waliyokuwa wanatumia ilikuwa imeshaharibiwa na mafuriko lakini kwa sasa kero hiyo imewaepuka baada ya kupata kibali cha serikali ya mtaa huo cha kurekebishiwa barabara hiyo.

Aidha Bw.John Nguvula amesema kuwa wamejitolea kutengeneza barabara hiyo kwani ilikuwa inahatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo hasa watoto wanaoenda shule,hivyo ameishukuru serikali ya mtaa wa Olorieni kuwapa kibali cha kutengeneza barabara hiyo mpaka kufanikiwa.






MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akifungua mkutano wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi uliofanyika mapema jana katika viwanja vya mbagala zakim jijini Dar-es-salaam.


  
Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimkaribisha mgeni rasmi makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.
                                                             


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hasssan akiangalia chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi baada ya kukabidhiwa na wataalamu wa masuala ya afya,wa kwanza kushoto ni waziri wa afya,maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto Mhe,Ummy Mwalimu.

Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu akipokea sindano ya chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kutoka kwa mtoa huduma za afya.kulia ni waziri wa afya maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe,Ummy Mwalimu.


Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu akipokea sindano ya chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kutoka kwa mtoa huduma za afya.kulia ni waziri wa afya maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe,Ummy Mwalimu.






   Picha ya pamoja ikionesha baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi waliohudhuria kumuunga mkono Mhe makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan wakatiwa uzinduzi wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.




NA EUNICE ROBERT
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan amezindua chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ili kutokomeza vifo vitokanavyo na magonjwa hapa nchini.

katika ufunguzi huo uliofanyika jana tarehe kumi mwezi wa nne jijini Dar-es-salaam makamu wa Rais Mhe,Samia amesema kuwa chanjo hiyo imewalenga wasichana wote wanaotimiza umri wa miaka 14 ili kuanza kujikinga mapema na ugonjwa huo.

"ili kupata kinga kamili,wasichana wanahitajika kupata dozi mbili ambapo dozi ya kwanza itatolewa muda wowote binti anapofikisha umri wa miaka 14 na dozi ya pili itatolewa muda wa miezi sita baada ya kupata dozi ya kwanza"alisema Mhe,Samia Suluhu.

Aidha Mhe,Samia amesema kuwa chanjo hiyo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi inatolewa bila ya malipo pamoja na uchunguzi wake kwani serikali imedhamiria kutokomeza tatizo hilo nchini.

"Niwaagize waganga wa mikoa na wilaya kuandaa kambi za wazi angalau mara tatu kwa mwaka ili kutoa huduma hiyo tena bila ya malipo kwa wanawake na wasichana wote mchini"alisisitiza makamu wa Rais Mhe,Samia Suluhu.
\
Mbali na hayo Mhe,Samia Suluhuamesema kuwa takribani wasichana laki sita kumi na sita elfu mia saba thelathini na nne wanatarajia kupata chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kwa mwaka 2018 na chanjo hiyo imethibitishwa na shirika la afya duniani (WHO).

Kwa upande wake waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe,Ummy Mwalimu amesema kuwa chanjo hii itakuwa ya saba kati ya chanjo ambazo zinatolewa kwa watoto ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali.

"Ukiacha chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi hapa nchini chanjo nyingine zinazotolewa ni ya kifua kikuu,polio,nimonia,kuharisha ama rota,surua na rubella,donda koo,kifaduro,homa ya ini,uti wa mgongo na pepopunda kwa watu wazima "alisema waziri Ummy.

Aidha waziri Ummy amesema kuwa serikali imefanikiwa kuweka maghala kuhifadhia chanjo katika mikoa yote nchini ambayo yana uwezo wa kuhifadhi chanjo kwa miezi sita bila ya kuharibika.

Kwa mujibu wa waziri Ummy amesema kuwa zawadi za fedha taslimu zitatolewa kwa mikoa mitatu itakayofanya vizuri katika utoaji wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi hapa nchini.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam Mhe,Paul Makonda amesema kuwa wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kwenda kupata vipimo na chanjo za kukinga saratani pindi wanapogundulika wana magonjwa hayo

"Natoa rai kwa wananchi mliojitokeza hapa kuwapeleka watoto wenu,wake zenu na wanawake wote hususani wasichana wenye umri wa miaka 14 kwenda kupata chanjo hii na mkifika majimbani kwenu muwakumbushe watu wenu wa karibu kushiriki katika upataji wa chanjo hii"alisema Mhe,Makonda.


Monday, April 9, 2018

RAIS MAGUFULI ATIMIZA AHADI YAKE KATIKA KANISA LA MTAKATIFU TERESIA JI...



NA EUNICE ROBERT

Katibu tawala mkoa wa Arusha Mh.Richard Kwitega amekabidhi mchango wa mifuko mia tatu ya sementi kwa ajili ya shughuli ya ujenzi wa Cathedral alioahidi Mh.Raisi John Pombe Joseph Magufuli siku ya tarehe nane katika sherehe za kumsimika Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Arusha Izack Amani.

Bw. Richard amesema kuwa amewasilisha mchango huo wa mifuko mia tatu ya sementi kwa niaba ya ikulu na kukabidhi kwa uongozi wa kanisa hilo kwa ajili ya kuwezesha kuendeleza ujenzi wa kanisa hilo lenye uwezo wa kuchukua takribani watu elfu tatu(3000)

Ameendelea kusema kuwa mchango wa rais Magufuli ni mkono mkubwa wa kuwezesha kukamilisha kanisa hilo na kuwaleta wakristo pamoja na kuwa mfano kwa viongozi wengine kuweza kujitoa kwa hali na mali kukamilisha ujenzi wa cathedral hiyo.

kwa upande wake katibu wa kamati ya ujenzi wa kanisa hilo Bw. Daniel Laizer amesema kuwa wamefurahishwa na kasi ya msaada huo na kumshukuru rais Magufuli kuonyesha mfano na pia wanaamini kuwa wengine watafwata kutoa michango yao.

Nae  paroko wa parokia hiyo ya mtakatifu teresia wa mtoto Yesu Bw. Paul Malisa amesema kuwa rais Magufuli aliahidi kutoa mifuko mia tatu ya saruji akiwa kama kiongozi mkubwa wa nchi anayependa maendeleo lakini pia kama muumini wa kanisa katoliki nae ameshiriki kwa nafasi yake kama waumini wengine wanavyochangia

amehitimisha kwa kusema kuwa wanamuombea rais kuweza kufanikiwa kwenye uongozi wake Mungu amjalie afya njema aweze kuwahudumia watanzania wote bila ubaguzi.


MAAFA ARUSHA: mafuriko yasababisha hasara kubwa kwa baadhi ya wakaz wa m...



NA EUNICE ROBERT

Pamoja na serikali kuendelea kutengeneza mikondo ya maji ili kuepusha mafuriko lakini bado baadhi ya maeneo mkoani Arusha yameendelea kukumbwa na adha ya mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa mtaa wa Lolovono mkoani humo wameeleza kile kilichotokea usiku wa kuamkia leo na kusema kuwa mvua zilizonyesha zimesababisha uharibifu mkubwa na kupoteza vitu vya ndani pamoja na kukosa mahali pa kulala kwani magodoro na vitanda vimechukuliwa na mafuriko hayo.

kwa upande wake Bi Dora John  mhanga wa tukio hili amesema kuwa mafuriko hayo yamesababisha nguo za watoto wake kulowa na kupelekea kukosa nguo za kuwavalisha watoto wake pamoja na kukosa mahali pa kulala kwani nyumba zimebomoka na magodoro yamelowana.

Nae Bi Irene Izack shuhuda wa tukio hili amesema kuwa mafuriko hayo yameanza jana usiku muda wa saa nane ambapo walishtushwa na kelele zilizowafanya waweze kutafuta msaada wa haraka kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko hayo

wakazi hao wamehitimisha kwa kuiomba serikali iwasaidie kurekebisha mkondo wa maji kwani maji hayo yalizidi na kukosa njia ya kutokea hivyo yalitafuta njia iliyoko wazi ambapo kuna makazi ya watu na kusababisha uharibifu wa mali zao.

Friday, April 6, 2018

SERIKALI YAWATAKA WAWEKEZAJI KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA UJENZI WA VIWANDA VYA DAWA.



WAZIRI WAAFYA MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO UMMY MWALIMU AKIWA
ANAZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA KUHAMASISHA UANZISHWAJI WA VIWANDA VYA DAWA


WAZIRI WA VIWANDA ,BIASHARA NA UWEKEZAJI MH.CHARLES MWIJAGE AKIWA ANAZUNGUMZA


NA EUNICE ROBERT

Serikali yawataka Wadau wa Uwekezaji nchini kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa ili kusaidia kupunguza gharama kubwa za matumizi zinazotokana na kununua, kusafirisha na kuhifadhi dawa zinazotoka nje ya nchi.


Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe.  UMMY MWALIMU  katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini, kilichokutanisha wadau mbalimbali wa Uwekezaji katika Sekta ya Dawa, Vifaa na Vifaa tiba


Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imekuwa ikitumia zaidi ya trilion moja kununua dawa kutoka nje, hivyo kupitia uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini itasaidia kupunguza adha hiyo nchini kwa kiwango kikubwa.

Nae Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Mhe. Charles Mwijage amewataka wote wenye nia ya kuwekeza katika Ujenzi wa viwanda vya dawa, vifaa na vifaa tiba lazima wahakikishe wanashirikiana na taasisi za Utafiti zilizopo nchini ili kuangalia mahitaji na aina ya dawa zinazohitajika.



AidhaMhe. Charles Mwijage amehitimisha kwa kusema  kuwa Uwekezaji na ujenzi wa Viwanda nchini utasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuchochea Maendeleo ya ukuaji wa Uchumi katika ngazi ya watu na taifa kwa ujumla.

Thursday, April 5, 2018

MAGUFULI KUZINDUA NYUMBA ZA POLISI ZILIZO JENGWA BAADA YA KUUNGUA MWAK...





NA EUNICE ROBERT

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kufungua kituo cha polisi cha kisasa cha kwanza hapa nchini siku ya jumamosi  kitakachotoa huduma kwa watalii na wanadiplomasia jijini Arusha.

Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa pamoja na mambo mengine raisi atazindua nyumba za askari zilizopo kituo cha polisi cha kati.

Bw.Charles ameendelea kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na maonyesho ya utendaji kazi wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha yatakayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid  hivyo ametoa wito kwa wananchi na wakazi wa Arusha kufika bila kukosa ili kushuhudia uimara wa jeshi la polisi.

Aidha ameongeza kuwa nyumba za polisi zimekamilika na mara baada ya kufunguliwa zitaanza kutumika pia ameendelea kusema kuwa kutafanyika ufunguzi wa vituo viwili vya polisi kwani hapa nchini Tanzania hakujawahi kuwa na kituo cha kidiplomasia hivyo amesema kuwa jeshi la polisi limeamua kufungua kituo kikubwa  cha kisasa kitakachofunguliwa na Mh.raisi John Pombe Magufuli.

Amehitimisha kwa kusema  kuwa kituo kingine cha kisasa cha daraja la kati ambacho kitatoa huduma kata ya Murieti kwa Morombo kitafunguliwa siku hiyo hivyo amewataka wananchi kuhudhuria siku hiyo kwa ajili ya kushuhudia ufunguzi wa nyumba hizo na utendaji kazi wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha.






Interested for our works and services?
Get more of our update !